Mwalimu ajinyonga kisa Wivu wa Mapenzi Muheza



Mwalimu Enock Johnson Peter (32) wa Shule ya Msingi Potwe wilaya ya Muheza Mkoani Tanga amekutwa amefariki dunia nyumbani kwake baada ya kujinyonga na shuka chanzo kikitajwa ni wivu wa kimapenzi.

Akithibitisha kutokea kwa Tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga (ACP) Almachius Mchunguzi amesema tukio hilo lilitokea Jumanne ya Julai 15,2025 katika kata ya Potwe, wilaya ya Muheza na uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo ni wivu wa kimapenzi.

Kwa upande wake Mratibu Elimu Kata ya Pongwe Rajabu Msuya leo Jumatano Julai 16,2025 alifika shuleni hapo kwaajili ya kikao na walimu wa shule hiyo ya Potwe ambapo walimu wote walikuja kwenye kikao, ila Enock hakutokea.

Amesema baadae alipotumwa mwanafunzi kwenda kumuita na aligonga mlango bila kuitikiwa na mwanafunzi kurudisha majibu hayo kuwa hakuna mtu anaitikia na kupo kimya iliwanidi kuagiza mwalimu mwingine kwenda kumuita mwenzao kwaajili ya kikao,ambapo na yeye alikosa majibu na kuamua kuchungulia dirishani na kubaini alikuwa tayari amejinyonga.

Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo Abdulrazaq Kikungo amesema siku mbili kabla ya marehemu kujinyonga aligombana na mwenzi wake na kutishia kumuua kwa kumchoma kisu baada ya kukuta meseji za kimapenzi kwenye simu ya yake na katika tukio hilo ndio alikimbia.

Mwili wa mwalimu umeagwa leo Jumatano shuleni hapo na kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao Ngara Kagera kwaajili ya shughuli za mazishi.

C