Mwanaharakati Agather Atuhaire Apatikana Mpaka wa Tanzania na Uganda

Mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka Uganda, Agather Atuhaire, ambaye alizuiliwa nchini Tanzania mapema wiki hii, amepatikana karibu na mpaka wa Mutukula unaotenganisha Uganda na Tanzania. Taarifa hizo zimethibitishwa na familia yake pamoja na marafiki zake, huku kituo cha televisheni cha NTV kikiripoti tukio hilo.

Atuhaire alikamatwa akiwa pamoja na mwanaharakati mashuhuri wa Kenya, Boniface Mwangi, walipokuwa wakielekea kushiriki kesi ya kiongozi wa upinzani wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu, nchini Tanzania.