Ngugi wa Thiong’o, mmoja wa waandishi mashuhuri wa fasihi kutoka Kenya, amefariki dunia leo, Jumatano, tarehe 28 Mei 2025, akiwa na umri wa miaka 87. Taarifa za kifo chake zimetolewa na binti yake, Wanjiku wa Ngugi, kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Katika taarifa hiyo, Wanjiku aliandika kwa hisia kuwa:
“Ni kwa huzuni kubwa tunatangaza kifo cha baba yetu, Ngũgĩ wa Thiong’o, asubuhi ya leo, Jumatano tarehe 28 Mei 2025. Aliishi maisha kamili, alipigana vita nzuri. Kama alivyotamani kabla ya kifo chake, tusherehekee maisha yake na kazi yake.”
Ngugi alitambulika sana kwa kazi zake zenye mguso wa kijamii na kiutamaduni kama vile The River Between, A Grain of Wheat, na This Time Tomorrow. Alijenga jina lake kama mmoja wa vinara wa fasihi afrika.
Kifo cha Ngugi wa Thiong’o ni pengo kubwa kwa tasnia ya fasihi, hasa barani Afrika, ambako mchango wake umeacha alama isiyofutika
Leave a Reply