Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Amani Golugwa, ameachiwa kwa dhamana usiku huu baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi saa 12:45 jioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3), alipokuwa akijiandaa kusafiri kuelekea Brussels, Ubelgiji.
Wadhamini wake, waliokamatwa walipofika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kumdhamini, pia wameachiwa. Wote wametakiwa kuripoti polisi tena kesho.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, Golugwa alikamatwa kutokana na taarifa za siri zinazodai kuwa amekuwa akisafiri nje ya nchi bila kufuata taratibu za kisheria. Taarifa hiyo ilithibitishwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Faustine Mafwele.
Leave a Reply