Navy Kenzo Wabadili Jina La Usanii

Kundi La Muziki Nchini La @navykenzoofficial Wametangaza Rasmi Kubadili Jina Lao Kutoka ‘Navy Kenzo’ Hadi ‘Aika & Nareel’.

Kupitia Ukurasa Wao Wa Instagram Wamethibitisha Hilo Kwa Kutoa Taarifa Iliyosomeka; 👇

“KUBADILI JINA KUTOKA NAVY KENZO KUITWA “AIKA & NAHREEL”

Tangu mwanzo wa safari yetu ya muziki, mmekuwa nasi mkitupa moyo, nguvu, na mapenzi yasiyoisha.

Leo tunatangaza rasmi kwamba jina letu la kisanii “Navy Kenzo” linafika mwisho wake, na tunaanza ukurasa mpya tukitwa: Aika & Nahreel.

Hatubadili kiini cha muziki wetu, bali tunaufanya uwe wa karibu zaidi, halisi zaidi, na wa kweli kwetu kama wasanii na watu binafsi. Kwa wote mlioamini katika sisi, mkashika mikono yetu na kutembea nasi, tunawashukuru kwa dhati.

Upendo wenu ndiyo umetufikisha hapa. Na upendo wenu huo huo ndio unatusukuma katika sura hii mpya.

Yours Truly,
Aika & Nahreel” – Navy Kenzo

JE, Una Maoni Gani Hapa ⁉️