Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amewataka Wakala wa Kuagiza Mafuta kwa Pamoja( PBPA) kuhakikisha uwepo wa akiba ya kutosha ya mafuta nchini ili kuhakikisha uendelevu wa shughuli za uzalishaji, usafirishaji na huduma nyingine muhimu zizotegemea nishati hiyo.
Mhe. Ndejembi ameyasema hayo Leo Novemba 25,2025 Dar es Salaam katika ofisi za PBPA ikiwa nimuendelezo wa ziara yake ya kuzungumza na viongozi wa Taasisi zilizoko chini ya Wizara ya Nishati.
“Akiba ya mafuta ya kutosha kupitia uwekezaji katika vituo vya kuhifadhi kunaleta utulivu wa kiuchumi kwa Taifa kwani kunapokuwa na uhakika wa upatikanaji wa mafuta, shughuli za uzalishaji, usafirishaji na biashara zinaendelea bila vizuizi na hii huongeza imani ya wawekezaji, hupunguza gharama za dharura, na hatimaye kukuza ukuaji endelevu wa uchumi” Mhe. Ndejembi
Aidha Mhe. Ndejembi amewataka viongozi wa PBPA kuhakikisha wanawekeza zaidi katika kuimarisha miundombinu ya kupokelea mafuta na kuhifadhia mafuta ili kuboresha usalama na ubora wa bidhaa kwa maslahi mapana ya Taifa.
Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa kuagiza mafuta kwa pamoja Bw. Erasto Simon ameeleza kuwa Katika kuhakikisha ufanisi katika utendaji kazi PBPA imejiandaa kuunganisha mifumo itakayosaidia kutoa bei linganifu kwenye bandari zote ili kuleta ufanisi katika usambazaji wa mafuta.
















Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.