NEMC yakabidhi tuzo kwa mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeandaa na kukabidhi tuzo maalum kwa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa kusimamia mazingira katika sekta mbalimbali jambo ambalo wamesema linaleta heshima kubwa kwa taifa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu NEMC, Dkt. Immaculate Semesi, katika hafla ya Ufungaji rasmi wa Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) Julai 13, 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa.

NEMC wameipongeza Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania kwa kutenga siku maalum ya mazingira ambapo iliadhimishwa Julai Mosi mwaka huu pia kwa kuhamasisha uchumi wa kijani na matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.