Nyota wa zamani wa Barcelona na PSG anayekipiga huko Saudi Arabia kwenye klabu ya Al-Hilal, Neymar Jr (32), anakaribia kurejea Santos, klabu aliyokulia, huku mazungumzo yakiwa katika hatua za mwisho.
Nyota huyo wa timu ya taifa ya Brazil anatarajiwa kujiunga na Santos kwa mkataba wa muda mfupi, huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kutangazwa rasmi kwa uhamisho huo.
Neymar amewahi kuichezea Santos ya kwao Brazil kwa takribani miaka 10 kuanzia timu ya vijana mwaka 2003 hadi 2009 alipopandishwa timu ya wakubwa ambapo alicheza hadi 2013 alipojiuga na Barcelona na kujizolea umaarufu mkubwa duniani akiwa Lionel Messi na Luis Suarez kwa kuunda utatu ‘mtakatifu’ wa MSN.
Got a Questions?
Find us on Socials or Contact us and we’ll get back to you as soon as possible.