Nicki Minaj amchana Vibaya Jay-Z, Adai Pesa zake Za ‘Tidal’.

Nicki Minaj Ameamka Na JayZ Leo!! Kwani Anasema Kwamba Anamdai Jay-Z Kati Ya $100m – $200m baada ya Kuuzwa kwa mtandao wa Kusikiliza Muziki Wa Tidal 2021. Nicki Amedai Kuwa anapanga kutumia pesa hizo kuwasaidia mashabiki Zake (Barbz) kuwalipia ada za chuo na mikopo ya wanafunzi.

Nicki Anasema yeye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kumiliki sehemu ya platform hiyo na alipambana Sana Katika kuitangaza (Promote) Zaidi Ya Hata Beyonce Pale Ilipozinduliwa.

Anadai kuwa wakati Jay-Z aliuza ‘Tidal’ 2021 kwa kampuni ya Jack Dorsey ‘SQUARE’ kwa kiasi cha dola milioni 300, wasanii wengine walilipwa kati ya dola milioni 8 hadi 9 kila mmoja, lakini yeye hakuambulia hata Senti.

Pia Nicki anasema alipewa ofa ya $1M (Tsh Bil 2.6/=) ili anyamaze kuhusu sakata hilo, lakini alikataa. Hivyo Baada Ya Kuanika Hadharani Yote Hayo Mashabiki Zake Wameonesha Kumuunga Mkono Wakisema Kuwa Hajatendewa Haki, Kwani Nicki Alichangia Kwa Kiasi Kikubwa Katika Kulitengeneza Jina la Mtandao Wa ‘Tidal’

Jay-Z aliinunua TIDAL mwaka 2015 kwa kiasi cha ($56M), Kisha Akaja Kuuza hisa zake nyingi (majority stake) za mtandao huo kwa kampuni ya SQUARE ambayo mmiliki wake ni Jack Dorsey, Aliyekuwa CEO wa Twitter Kwa Kiasi Cha $297 (Tsh Bilioni 689+). Baadhi Ya Wasanii ambao walikuwa wamiliki Wenza Na Jayz wa mtandao huo Ni Alicia Keys, Beyonce, J. Cole, Kanye West, Lil Wayne, Rihanna, T.I, Nicki Minaj na wengine.