Nicki Minaj Awachana Jay-Z Na CEO Wa Roc Nation ‘Desire Perez’

Nicki Bado Anaendelea Kuwasha Moto!! Baada Ya Kudai Kudhulumiwa Malipo Ya Mtandao Wa ‘Tidal’ Na Jayz, Sasa Amewachana Jay-Z Na Mkurugenzi Wa Kampuni Ya Roc Nation ‘Desire Perez’.

Nicki amewashutumu Jay-Z na Desiree kwa unafiki wa kisiasa, akisema Jay-Z hakuwahi kujitokeza hadharani kumpigia kampeni ‘Kamala Harris’ au ‘Obama’, licha ya kunufaika na chama cha Democrats, huku akitilia shaka uhusiano wao na Rais Trump, aliyemsamehe Desiree Perez.

Kama Unakumbuka 2021 Kabla Ya Trump Kuachia Madaraka Alimsamehe Desiree Perez Ambaye Alikutwa Na Hatia 1994 Kwa Makosa Ya Biashara Za Dawa Za Kulevya na pia alikuwa anashirikiana na mamlaka kama informant (mtoa taarifa).

Wakati msamaha huo ulipotangazwa, watu wengi walishangazwa kuona Trump akimsaidia mtu wa Roc Nation, hasa ikizingatiwa kwamba kampuni hiyo Na Jay-Z waliwahi kuonekana kuwa karibu na upande wa Democrats.

Hivyo Nicki Amedai kuwa wawili hao wanaendelea kuwadanganya Wamarekani weusi kwa maslahi yao binafsi, Huku Akihitimisha Kwa Kuwachana Kuwa; Wameiharibu Game Ya Hiphop, Mpira (American Football), Mpira Wa Kikapu, IG Na Twitter.