Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano na vyuo vya ufundi na vya kati – 2025 (first selection)

Jumla ya wanafunzi 149,818 sawa na asilimia 69.96 wamechaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano, huku 64,323 wakichaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa, ameyasema hayo leo Juni 6, 2025, wakati akizungumzia kuhusu uchaguzi wa wanafunzi wa kidato cha tano na vyuo mbalimbali.

Alifafanua kuwa jumla ya wanafunzi 214,141, wakiwemo wasichana 97,517 na wavulana 116,624, walibainika kuwa na sifa za kuchaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi, ikiwemo wanafunzi 1,028 wenye mahitaji maalumu.

Bofya Hapa Kutazama Orodha kamili ya wanafunzi waliochaguliwa na fomu za kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi mwaka 2025. au Tembelea kwenye tovuti za Ofisi ya Rais – Tamisemi (www.tamisemi.go.tz) na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (www.nactvet.go.tz).