Papa Leo XIV ameongoza Misa katika Kanisa la Sistine, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo kama kiongozi wa Kanisa Katoliki.
Papa Leo XIV Mzaliwa wa Chicago alichaguliwa jana kuwa papa wa 267, kiongozi wa kiroho wa waumini bilioni 1.4 wa kanisa Katoliki, kufuatia mkutano maalumu wa makadinali wenzake katika makazi rasmi ya papa kanisa la Sistine mjini Vatican
Papa Leo amewahutubia Makardinali ambapo amewaambia kwamba anatumai kuchaguliwa kwake kunaweza kusaidia Kanisa Katoliki kuleta mwanga kwenye “usiku wa giza wa ulimwengu huu” na kwamba anaweza kuwa “msimamizi mwaminifu” wa Kanisa zima.
Papa Leo XIV aongoza Misa ya Kwanza kama Papa

Leave a Reply