Pogba amaliza adhabu yake, unatamani kumuona timu gani ?

Kiungo wa zamani wa Juventus na Manchester United, Paul Pogba (31) amemaliza adhabu yake ya kutocheza mpira kwa kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, ambayo awali ilikuwa ni miaka minne kabla ya CAS kupunguza adhabu hio na kuwa miezi 18

Kutokana na adhabu hiyo kupunguzwa, Pogba anatarajiwa kurudi uwanjani akiwa kama mchezaji huru baada ya klabu yake ya zamani Juventus kuvunja mkataba nae.