Polisi waeleza Sababu za Tundu Lissu kukamatwa, Ni “Uchochezi”

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amethibitisha kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu, kulikotokea jana, Aprili 9, 2025.

Kwa mujibu wa Kamanda Chilya, Lissu amekamatwa kutokana na tuhuma za kufanya uchochezi wa kutaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Mtuhumiwa huyo (Lissu) anaendelea kuhojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuhuma hizo.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa vyama vyote vya siasa kuepuka kutoa maneno ya uchochezi, lugha ya kukashifu polisi au serikali, au kuonesha viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu.