Polisi wamkamata Naibu Katibu Mkuu CHADEMA Bara, Sababu zatajwa

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limethibisha kumkamata Amani Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) tarehe 13/05/2025 majira ya saa 06:45 usiku katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere lango namba 03 (terminal 03) wakati akiwa katika maandalizi ya kusafiri
kuelekea Brussels Nchini Ubelgiji.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Jeshi hilo lilimkamata Naibu Katibu Mkuu huyo kufuatia taarifa za siri kuwa amekuwa na mienendo ya kuondoka na kurudi Nchini bila kufuata taratibu za kisheria hapa Nchini.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi
wa kina wa taarifa hizi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Usalama
kuhusu suala hilo.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati uchunguzi ukiendelea na kupuuza taarifa za upotoshaji kuhusu hatua hizi za kisheria zinazomhusu Amani Golugwa