Jeshi la Polisi limeeleza kuwa kuna taarifa za uongo, upotoshaji na zisizo na maadili zilizokuwa zikisambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jeshi la Polisi (tanpol) kwa lengo la kutaka kuuaminisha umma kuwa zimetolewa na Jeshi la Polisi kupitia
mtandao wake wa X.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa Taarifa hizo si za kweli na kwamba Jeshi hilo haliwezi kuandaa na kusambaza taarifa kama hizo katika Mitandao yake ya kijamii
“Wakati tunaendelea kufuatilia wahalifu waliotengeneza na kusambaza taarifa hizo ili wakamatwe, tunawaomba wananchi wazipuuze taarifa hizo na kuepuka kuendelea kuzisambaza endapo zitakufikia.”
“Hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote yule aliyehusika na utengenezaji na utoajiwa tarifa hizo na yeyote yule ambaye ataendelea kuzisambaza” – Imeeleza Taarifa ya Polisi
Leave a Reply