Polisi Zanzibar wafunguka upelelezi kifo cha Sheikh Jabir Haidar

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharib Unguja kupitia kwa kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi SACP Richard Thadei Mchomvu limesema linaendelea na upepelezi wa kubaini chanzo hasa cha kifo cha Shekh Jabir Haidar ambaye mwili wake ulikutwa pembezoni mwa barabara usiku wa kuamkia Mei 28, 2025

Kamanda Mchomvu ameeleza hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa wasafi aliyetaka kufahamu upelelezi wa tukio hilo umefikia wapi, ambapo kamanda huyo alisema mpaka sasa wamefikia pazuri ambapo muda mchache watatoa taarifa rasmi juu ya chanzo cha kifo hicho

Hapo jana Mei 31, 2025 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman aliongoza mamia ya waumini wa Kiisalamu katika kisomo maalum cha Dua kwaajili ya Marhemu Shekh Jabir Haidarz hafla ya dua hiyo imefanyika katika Msikiti wa Weles Zanzibar