Waziri wa Elimu, Sayansi na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Adolf Mkenda ametoa Rai kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, VETA, kuhakikisha kwamba inashirikina na Taasisi za Umma na Binafsi zilizopo kwenye Mnyororo mmoja ambao unasimamiwa na Mamlaka hiyo, lengo likiwa ni Kufahamu Vizuri Uhitaji wa Soko, Changamoto na namna nzuri ya kuboresha eneo pana la Ufundi Stadi hapa nchini.
Profesa Mkenda ametoa kauli hiyo leo Jijini Dar es Salaam Machi 14, 2025 katika kikao chake na Wadau kwenye Sekta ya Nguo na Mavazi kupitia Kongamano lililoandaliwa na Mamlaka ya Elimu ya Ufundi Stadi ikiwa ni Katika kuelekea miaka 30 tangu kuanzishwa kwa VETA.
“Ninachotaka kusema hapa ni kwamba ili kufikia lengo la Serikali, kuzalisha nguvu kazi ya Taifa kupitia Kundi la Vijana ambao wanaweza kulikabili Soko la Ajira, ni muhimu kwa Mamlaka ya Veta, kujenga mahusiano yaliyo bora na Taasisi hizo kwa Muktadha wa Kubaini kinachohitajika Sokoni” amesema Profesa Adolf Mkenda.
Leave a Reply