Idara ya Uhamiaji imewaondosha nchini raia wawili wa kigeni baada ya kubainika wamekiuka masharti ya viza zao za matembezi. Wageni hao ni Dkt. Brinkel Stefanie, raia wa Ujerumani mwenye hati ya kusafiria namba C475MMNGL, na Bi. Catherine Janel Almquist Kinokfu, raia wa Marekani mwenye hati ya kusafiria namba A80321764.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Idara hiyo SSI. Paul J. Mselle hatua hiyo imechukuliwa tarehe 13 Oktoba 2025 baada kubainika kuwa wageni hao walikuwa wamekiuka masharti ya viza walizopewa wakati wa kuingia nchini.
Aidha, Idara ya Uhamiaji imetoa wito kwa raia wa kigeni wanaoingia na kuishi nchini kwa madhumuni mbalimbali kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika viza au vibali vyao kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura 54 pamoja na Kanuni zake ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza pindi wanapokiuka sheria
Leave a Reply