Mwanasiasa mkongwe wa Kenya, Raila Amolo Odinga ambaye ni mmoja wa watu mashuhuri zaidi katika historia ya siasa za nchi hiyo na mtetezi wa muda mrefu wa demokrasia amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.
Odinga aliyewahi kuwa Waziri Mkuu Wa Nchi hiyo amefariki Jumatano wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja nchini India. Kifo chake kinakuja baada ya tetesi zilizodai kwamba hali yake ilikuwa mahututi.
Leave a Reply