Rais Dkt. Mwinyi ateua Bosi Mpya ZRA

RAIS WA ZANZIBAR AMTEUA SAID KIONDO ATHUMANI KUWA KAMISHNA MKUU WA ZRA

Zanzibar, Tanzania – Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amemteua Said Kiondo Athumani kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar (ZRA). Uteuzi huu unafuatia mabadiliko ya uongozi ndani ya mamlaka hiyo, ambapo Kamishna wa zamani wa ZRA, Yusuph Mwenda, sasa anashikilia wadhifa wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hii, Bwana Said Kiondo Athumani alikuwa mkufunzi katika Chuo cha Kodi cha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Uteuzi huu ni sehemu ya juhudi za serikali ya Zanzibar katika kuimarisha usimamizi wa mapato na kuleta ufanisi ndani ya Mamlaka ya Mapato Zanzibar. Wananchi na wadau wa sekta ya kodi wanatarajia kuona maboresho zaidi katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi wa rasilimali za Zanzibar chini ya uongozi wake.