Rais Mwinyi akutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameishukuru  Serikali ya Uingereza kwa kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kuboresha miundombinu ambapo hivi karibuni Taasisi ya UK Export Finance ya Uingereza imetoa dhamana kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pemba pamoja na miundombinu ya Barabara Unguja na Pemba.



Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Naibu Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe.Angela Rayner tarehe 8 Aprili 2025, Jijini  London.

Naye, Mhe.Rayner ameeleza kuwa Serikali ya Uingereza imeweka kipaumbele cha kukuza uchumi  ambapo kupitia mahusiano na mataifa rafiki itakuwa tayari kukuza biashara na uwekezaji Zanzibar.

Halikadhalika, Tanzania na Uingereza zakubaliana kukuza zaidi ushirikiano katika biashara na uwekezaji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa Mutual Prosperity Partnership, makubaliano hayo yamefikiwa  tarehe 8 Aprili 2025 wakati wa mazungumzo baina ya Rais Dkt.Mwinyi na Naibu Waziri Mkuu huyo Jijini London.