Rais Samia ateua mrithi wa Prof. Janabi Muhimbili

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wapya na kumpangia kituo cha kazi Balozi. Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imefafanua uteuzi huo kama ifuatavyo:

  • Dkt. Delilah Charles Kimambo ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Dkt. Kimambo anachukua nafasi ya Profesa Mohamed Yakub Janabi aliyechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika.
  • Jaji Mstaafu Hamisa Hamis Kalombola ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha pili.
  • Bwana Paul Thomas Sangawe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa SELF kwa kipindi cha pili.
  • Jaji Rose Ally Ebrahim ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal).
  • Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amepangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.