Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema kufuatia hatua za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua mipaka ya nchi kiuchumi, wizara imejikita katika kuhakikisha inaboresha miundombinu ya minada ili bidhaa zitokazo katika minada hiyo zifikie viwango vya kimataifa.
Waziri Mhe. Dkt. Kijaji amebainisha hayo leo (08.01.2025) wakati alipotembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa mnada wa awali wa Kata ya Lunguza uliopo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga ambapo amesema mnada huo ambao unawekewa miundombinu yote muhimu utaleta tija kwa wafugaji kwa kupata masoko kutokana na mnada huo kuwa wa kisasa.
Ameongeza kuwa serikali imetenga fedha Shilingi Milioni 399 na tayari mkandarasi amefikia asilimia 90 ya ujenzi huo na kulipwa asilimia 40 ya gharama ya mradi huo huku akiahid fedha zilizobaki kulipwa mwezi huu ili mkandarasi akamilishe ujenzi wa miundombinu iliyobaki.
Rais Samia amefungua Biashara Kimataifa, Wafugaji Changamkieni Fursa – Waziri Kijaji
![](https://wasafimedia.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/Screenshot-2025-01-08-192911.png)
Leave a Reply