Rais Samia aomboleza Kifo cha Papa Francis

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, kilichotokea leo, Jumatatu, Aprili 21, 2025, Vatican.


Rais Samia amesema kuwa katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani.


“Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote,” amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Ameongeza kwa kumuomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Papa Francisko mahali pema Peponi, Amina.