Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kupokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mheshimiwa Raila Amolo Odinga kilichotokea leo Oktoba 15, 2025 wakati akipatiwa matibabu nchini India
Rais Samia amesema kuwa Odinga alikuwa kiongozi mahiri, Mwanamajumui wa Afrika, mpenda amani na mtafuta suluhu, ambaye ushawishi na upendo wake haukuwa tu ndani ya Kenya, bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
“Msiba huu si wa Kenya pekee, bali wetu sote. ” – Dkt. Samia
Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia ametuma salamu za pole kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Dkt. William Samoei Ruto, Mama Ida Odinga, watoto, familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wote wa Kenya kwa msiba huu.
“Tunaungana kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na imani katika kipindi hiki, na ailaze roho ya mpendwa wetu, Mheshimiwa Raila Amolo Odinga, mahali pema peponi. Amina.” – Rais @Samia_Suluhu_Hassan
Leave a Reply