Rais Samia azindua Jengo la Makao Makuu ya Mahakama Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza
umuhimu wa Mahakama, hususan Mahakama za Mwanzo kutokufungwa na masharti ya
kiufundi katika utoaji haki ili kurahisisha upatikanaji wa haki na kuzidi kujenga imani kwa
wananchi kuwa Mahakama ndio kimbilio lao kuu katika kudai haki.

Rais Dkt. Samia amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Jengo Ja Makao Makuu ya
Mahakama ya Tanzania uliyofanyika katika eneo la Tambukareli, jijini Dodoma

Rais Dkt. Samia amesisitiza umuhimu wa jengo hilo lililogharimu Shilingi Bilioni 129.7
kutunzwa na kutumika ipasavyo na umuhimu wa ubora wa huduma zinazotolewa
kuendana na ubora wa uwekezaji uliofanywa kwenye jengo hilo

bambamba na hilo, Rais Dkt. Samia amezindua miradi mingine miwili ikiwemo jengo jipya
la ghorofa sita la Tume ya Utumishi wa Mahakama, pamoja na nyumba 48 za kisasa za
makazi ya Majaji zilizopo jijini Dodoma.

Aidha, katika kuhakikisha haki inapatikana kwa wote na kwa wakati, Rais Dkt. Samia
alieleza haja ya Mahakama ya Tanzania kuendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA
katika kutoa huduma za kimahakama ili kuendana na kasi ya dunia, kurahisisha uendeshaj
wa mashauri na upatikanaji haki,

Rais Dkt. Samia pia amesisitiza umuhimu wa kuimarisha Mahakama Maalum
zinazoshughulikia masuala ya ardhi, familia na biashara ili nazo zitoe huduma bora na
kuchangia ukuaji wa sheria kwenye maeneo yao,

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amepongeza utendaji kazi wa Jaji Mkuu wa
ľanzania, Profesa Ibrahim Juma kwa kuitumikia nafasi hiyo kwa ufanisi na uzalendo na
kuleta maboresho makubwa kwenye Mahakama

Kwa mara ya kwanza katika historia ya miaka 104 ya uwepo wake, Mahakama ya Tanzania
sasa ina Makao Makuu yenye hadhi. Aidha kwa Mahakama ya Tanzania kuhamia rasmi
Mkoani Dodoma kunafanya mihimili yote mitatu ya Serikali kuwepo makao makuu ye
nchi.