Rais Samia: Sijawahi kutoa Maelekezo mtu asilipe Kodi

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameeleza kwamba hajawahi kutoa Maelekezo kwa Mtu, Kikundi ama Taasisi yoyote isilipe kodi Stahiki, kwa Sababu Ulipaji Kodi ni takwa la Kisheria.

Dkt Samia ametoa Kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya Utoaji tuzo kwa Walipa kodi Bora katika Kipindi cha mwaka 2023/ 2024, tuzo ambazo zimeratibiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Nataka niseme Jambo moja, kumekuwa na baadhi ya watu wanakwepa kodi kwa Kisingizio cha maelekezo kutoka Juu, Kwa Ilivyo maelekezo kutoka Juu ina maana ni Rais, kwa hiyo nachotaka kusema hapa Mimi kama Rais Sijawahi kutoa Maelekezo ya mtu asilipe kodi, Kodi ni lazima ilipwe kwa mujibu wa Sheria, na ikitokea hivyo basi maelekezo yangu lazima yaambatane na Maandishi” amesema Dkt Samia