Rapa Glorilla Akamatwa Na Dawa Za Kulevya.

Rapa wa Marekani GloRilla amekamatwa na polisi wa Georgia kwa tuhuma za kumiliki dawa za kulevya baada ya polisi kugundua kiasi kikubwa cha bangi na dawa nyingine nyumbani kwake kufuatia uchunguzi ulioanzishwa baada ya jaribio la uvamizi Wa Majambazi Nyumbani Rapa Huyo.

Ikiwa Glorilla Hakuwepo nyumbani wakati Uvamizi Wa Majambazi unatokea, Polisi Walioitwa Kwa Ajili ya uchunguzi wa tukio hilo nyumbani kwa Rapa huyo Walidai kusikia harufu ya marijuana, Kitendo kilichopelekea Kuanza Upekuzi.

Glorilla alijisalimisha polisi tarehe 22 Julai na aliachiwa kwa dhamana ya $22.2K (Tsh Milioni 57/=), huku mashabiki wake wakisubiri taarifa rasmi kutoka kwa timu yake ya sheria kwani tukio hili linaweza kuathiri ratiba na taswira yake kijamii.