Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila ameelekeza kuudwa kwa kamati maalum ambayo itafanyakazi kwa muda wa siku tatu kuanzia julai 21 hadi 23 kushughulikia mgogoro umiliki wa uwanja wa Sahara kati ya wananchi wa mtaa wa mabibo na Saccos ya wafanyakazi wa shirika la posta na simu ambapo pande zote zinadai kuwa ni wamiliki halali
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sahara uliopo Mabibo Wilaya ya Ubungo RC Chalamila amesema lengo la kamati hiyo ni kijiridhisha uhalali wa vielelezo na maelezo yaliyotolewa na pande zote mbili kabla ya kutoa uamuzi hivyo anahitaji kamati hiyo kujumuisha wananchi, wanaushirika wa Sacoss ya shirika la posta na simu pamoja na wataalamu kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
Aidha RC Chalamila amehimiza wananchi kuwa na utamaduni wa kuwa na nyaraka za umiliki wa ardhi yaani hati badala ya maelezo ya mdomo kwani kukosekana kwa nyaraka kunaweza kupelekea mtu kupoteza haki yake.
Awali kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Wakili Albert Msando ametoa taarifa ya mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka 30 tokea mwaka 1994 ambapo amesema kwa mujibu wa nyaraka zilizopo zinaonesha eneo hilo linamilikiwa na Sacoss ya wafanyakazi ya shirika la posta na simu

Leave a Reply