Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ameuagiza Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Amana kushughulikia madai ya Bi Martha Lazi, kwa kuanza kuchunguza nyaraka na Viambatanisho muhimu kwa lengo la kujiridhisha kama anastahili kulipwa Fedha zake kulingana na makubaliano ya Mkataba.
RC Chalamila ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salam leo Machi 11, 2025 alipofika katika Hospitali ya Amana Baada ya Kusambaa kwa ‘Video Clip’ katika Mitandao ya Kijamii ikimuonesha Bi Martha akieleza kuidai Hospitali hiyo Fedha kama malipo Baaada kukamilisha Tenda ya Kupelekea Pazia na nguo katika Chumba cha Upasuaji.
Bi Martha akizungumza Mbele ya RC Chalamila alieleza kudai kiasi cha Zaidi ya Shilingi Milioni 5 kutokana na kazi hiyo ambayo aliifanya kati ya mwaka 2019 na 2021.
Akielezea Kuhusiana na Sakata hilo RC Chalamila ameuagiza Uongozi wa Hospitali hiyo Kupitia kwa Mganga Mfawidhi Dkt Bryceson Kiwelu kuharakisha Uchunguzi wa Suala hilo ili kuona kama Bi Martha anastahili kulipwa kulingana na Nyaraka zilizopo na Taratibu za Kiserikali kulingana na Matumizi ya Fedha za Umma.
“Tumekwishamuelekeza mganga mkuu katika Hospitali hii ya Amana kuanza Uchunguzi wa mara moja pamoja na Uthibitisho wa nyaraka zilizowa silishwa na Bi Martha ili pale anapostahili aweze kulipwa Fedha zake” amesema RC Chalamila.
Kwa Upande wa Bi Martha Lazi akizungumza Baada ya Maelekezo na Ufafanuzi Uliotolewa na RC Albert Chalamila, ameeleza kuridhishwa na Maelezo ya Mkuu wa mkoa na Ushauri ambao ameupata katika kupata haki yake.

“Naomba Niwaambie Watanzania kwa Kufuatia Video Clip yangu iliyoruka Machi 8 mwaka huu, ni kweli ninaidai Amani lakini nimebaini kwenye mkataba wangu kuna vitu vilikuwa havijakaa Sawa, lakini nashukuru Nimeeleweshwa vizuri” amesema Bi Martha.
Nae Mganga Mfawidhi katika Hospitali ya Amana Dkt Bryceson Kiwelu ameeleza kupokea maagizo ya Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila kuhusu Suala la Bi Martha, huku akieleza kwamba yote yanaanza kufanyiwa kazi mara moja ili kila Upande Upate Haki inayostahili.
Keep on writing, great job!