Rick Ross Amjibu 50 Cent, Adai Kununua Haki Za Muziki Wake.

Baada ya Rapa 50 Cent kudai kuwa Rick Ross Anaenda Kufungua Show Ya “Bow Wow” Kwenye Ziara Ya Millennium Tour Kwa Kiasi Cha $30K (Tsh Milioni 79.3/=) Na Kwamba Hawezi Hata Kuuza Tiketi, Rick Ross Ameibuka Na Kumjibu kwa kejeli Kupitia IG Story (Video) akisema anapanga kununua haki miliki za muziki Wa 50 Cent.

Mbali na hilo, Rozay pia amehoji kuhusu mafanikio ya studio za filamu za G-Unit, akitilia shaka maendeleo ya Miradi ya 50 Cent katika sekta hiyo. Rozay Anasema 50 Ameshindwa Kuendeleza Kabisa Studio Hizo.

Tofauti za wawili hao zilianza mwaka 2008 na walifika hatua hadi za kushambuliana kwa kupigana Risasi miaka kadhaa iliyopita.