Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mudrick Ramadhan Soraga amesema ujio wa magwiji wa mchezo wa mpira wa Miguu kutoka Brazil ukiongozwa na Ronaldinho Gaucho kutaongeza kasi ya ukuaji wa watalii na kufikia watalii Milioni moja na Laki tano kwa mwaka
Waziri Soraga ameeleza hayo wakati wa kutoa taarifa ya ujio wa Magwiji hao wa Mpira wa miguu kutoka Brazil ambapo watacheza mechi ya kirafiki na magwiji wa mpira wa miguu Zanzibar Julai 27 mwaka huu katika uwanja wa New Amaan Compex Mjini Unguja
Amesema kwasasa sekta ya utalii imekua kwa kiasi kikubwa ambapo wastani wa watalii zaidi ya laki saba kwa mwaka ambapo lengo la serikali kufikia mwaka 2027 kupokea watalii Milioni moja na Laki tano kwa mwaka
Kwa upande wake Balozi mdogo wa Brazil Zanzibar Mheshimiwa Balozi Abdulswamad AbdulRahim amesema hatua hiyo ni sehemu ya kutekeleza adhma ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuchochea sekta ya utalii
Amesema katika Mtanange huo Mashabiki zaidi ya 18,000 watashuhudia mubashara na kuwafikia watazamaji zaidi ya Milioni Mia nane duniani kote kufatilia kupitia Televisheni
Leave a Reply