Kutokufanya kazi masaa 24 kWa kituo cha forodha upande wa Nakonde Nchini Zambia,kufungiwa kwa baadhi ya mawakala wa forodha kutokana kukosa sifa pamoja na upande wa Tunduma Tanzania baadhi ya wakala wa forodha kufanya udanganyifu na kuchelewesha nyaraka na ufinyu wa miundombinu ya barabara zimekuwa ni baadhi ya sababu ambazo zinasababisha msongamano wa malori katika Mpaka wa Tunduma ambazo zimebainika kufuatia kamati Maalum iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo.
Hayo yamebainika na kamati hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndugu Chesco Mbilinyi na kuwasilishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
Kufuatia changamoto hizo na mapendekezo yaliyotolewa na kamati hiyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameahidi kuzishughulikia changamoto hizo ikiwemo kufanya kikao na wizara zote zinazohusika na sekta ya usafirishaji pamoja na kufanya mazungumzo cha ujirani mwema na nchi jirani ya Zambia.
Leave a Reply