Sakata la kanisa la Gwajima, DC Msando aeleza kilichotokea

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikisema kuwa Jeshi la Polisi Wilaya ya Ubungo lilivamia Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Joseph Josephat Gwajima.

Amesema kilichofanywa na jeshi hilo ilikuwa ni kusimamia maelekezo ambayo kanisa hilo walipewa ya kusitisha kuendelea na huduma za ibada, baada ofisi ya kanisa kukataa kupokea barua ya mkuu huyo wa wilaya, ambapo pia waumini wa kanisa hilo walionekana kukaidi maagizo ya kusitishwa kwa huduma za kanisa kwa kuendelea kufanya ibada.