Kampeni ya Samia Teacher’s Mobile Clinic imezinduliwa rasmi mkoani Ruvuma, ikiwa na lengo la kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakumba walimu nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Angalikana mjini Songea leo Januari 16,2024.
Akizungumza katika uzinduzi huo, mgeni rasmi Bi. Merry Makondo, Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma, amesema kuwa jumla ya walimu 1,000 wamejitokeza kuwasilisha kero zao na kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na sekta ya elimu.
“uwepo wa huduma hii hapa mkoani kwetu umesaidia kuokoa rasilimali fedha na muda, kwani hapo awali walimu walilazimika kusafiri mpaka makao makuu ya Chama cha Walimu na wizara husika ili waweze kutatuliwa kero zao.”
Halikadharika Bi. Makondoa ametoa rai kwa maafisa watumishi wa Halmashauri mkoani humo kuendelea kukusanya kero za walimu na kisha kuzipeleka kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ili ziweze kufanyiwa kazi .
Kwa upande wake, Makamu wa Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Suleiman Komba, amesema kampeni hiyo inalenga kuwafikia walimu wote wenye changamoto.
“kwa kutumia huduma ya Samia Teacher’s mobile clinic, ni rahisi kwa kila mwalimu mwenye changamoto yoyote kufikiwa na kusaidiwa, na hivyo kuondoa vikwazo vya usafiri na upatikanaji wa huduma kwa walimu katika maeneo mbalimbali. Hii ni hatua muhimu katika kuboresha ustawi wa walimu na sekta ya elimu kwa ujumla
Leave a Reply