Sekta ya utalii iguse hali za uchumi kwa wananchi wa Zanzibar” – Waziri Soraga

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mheshimiwa Mudrick Ramadhan Soraga amesema serikali iko tayari kupokea mashauri ya mabadiliko ya kisera katika kutoa msukumo kwa wananchi hasa vijana kuwa tayari kunufaika na fursa zitokanazo na sekta ya Utalii nchini

Waziri Soraga ameeleza hayo wakati akishiriki katkam warsha ha utafiti wa masuala ya sera za kisiasa na uchumi ambayo inahusisha vyuo vikuu mbalimbali, hafla hiyo imefanyika katika Chuo cha ITT Madras Bweleo Zanzibar

Soraga amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana kutoka na uwekezaji kwenye sekta ya utalii bado kuna changamoto za vijana kushindwa kuzitumia fursa za ajira na kuajirika katika sekta hiyo hali inayopelekea kuzorota kwa hali za kiuchumi kwa wananchi wa Zanzibar

Amesema serikali iko tayari kuboresha sera zake katika kuhakikisha hali za uchumi kwa wananchi wa Zanzibar zinaimarika ili kuendana na hali ya uwekezaji wa sekta ya utalii Zanzibar

Katika uchumi wake jumla, sekta ya Utalii Zanzibar imekua ikichangia asilimia 30 ya pato la Taifa na asilimia 70 ya fedha za kigeni