Sera za Trump zawakutanisha wadau wa uchumi na biashara Zanzibar

PHOENIX, ARIZONA - DECEMBER 22: U.S. President-elect Donald Trump smiles during Turning Point USA's AmericaFest at the Phoenix Convention Center on December 22, 2024 in Phoenix, Arizona. The annual four day conference geared toward energizing and connecting conservative youth hosts some of the country's leading conservative politicians and activists. (Photo by Rebecca Noble/Getty Images)

Wataalamu wa masuala ya uchumi na biashara wamekutana Zanzibar kujadili namna ambavyo baadhi ya sera za Rais wa Marekeni Donald Trump zinavyoathiri uchumi wa Dunia

Majadiliano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Utafiti na sera za Umma Zanzibar ambayo yamefanyika katika ofisi zao zilizopo Vuga na kuongozwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mheshimiwa Dkt Saada Mkuya Salum

Dkt Mkuya akichangia kwenye mjadala huo amesema uamuzi wa Rais Trump kuongeza ushuru wa kodi kwa bidhaa zinatoka nje ya Marekani kumeathiri biashara mbalimbali za Zanzibar katika kuuza kwenye soko la nje

Katika kujikwamua na Hali hiyo Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mheshimiwa Omar Said Shaaban amesema ni vyema kuweka mikakati ya pamoja kwa bara la Afrika kuhakikisha bidhaa zinazodhalishwa zinasambazwa katika bara hilo na kuwa na soko la uhakika

Mkurugenzi wa Benki Kuu ya Tanzania Makao Makuu ndogo Zanzibar Ibrahim Malogoi amesisitiza matumizi ya mfumo wa uchumi kidigitali ukilenga mifumo ya malipo ya Kidigitali ili kuchochea ukuaji wa uchumi huku akisema kuwa benki Kuu imekuja na mfumo wa malipo ambao utapunguza gharama za ziada wakati wa kufanya miamala ya bidhaa