Familia ya Marehemu Christian Robert ambaye ni dereva wa masafa marefu, hatimaye imefanikiwa kuupokea mwili wa ndugu yao huyo aliyefariki kwa ajali nchini Congo takribani wiki mbili zilizopita.
Wakizungumza wakiwa kwenye mapokezi ya mwili huo ndugu wa Robert wameeleza kuwa ndugu yao alifariki kwa ajali katika eneo la Kasumbalesa Aprili 29 mwaka huu, ambapo baada ya jitihada za Serikali kwa kushirikiana na Chama cha Madereva kimefanikisha urudishaji wa mwili huo usiku wa kuamkia Mei 16, 2025, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Aidha, Mwenyekiti wa Chama cha Madereva wa masafa marefu Tanzania Hassan Dede amesema mbali na kifo cha dereva huyo hivi karibuni kumekuwepo na mfululizo wa vifo vya madereva wa masafa marefu nchini Congo kufariki katika mazingira ya kutatanisha wakiwa ndani ya Malori, jambo ambalo linawaacha na sintofahamu bila kupata majibu ya vyanzo vya vifo hivyo.
Dede ameiomba Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Congo kufanya uchunguzi wa kina wa vifo hivyo ili kujua sababu hasa inayopelekea, huku akisisitiza madereva kuwa na utaratibu wa kupima afya zao kabla ya kusafiri nje ya mipaka ya Tanzania ili kusaidia kupunguza au kumaliza matukio hayo, wakati Serikali ikiendelea kuchunguza.
Leave a Reply