Umoja wa Walimu Wasiokuwa na Ajira (NETO) umeeleza kuwa umefanikiwa kufanya mazungumzo na Serikali kuhusu changamoto ya ukosefu wa ajira kwa walimu, ambapo Serikali imetoa muda wa siku 30 hadi 45 ili kutoa majibu ya utatuzi wa tatizo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma, Mwenyekiti wa NETO, Mwl. Joseph Kaheza, amesema kuwa walikutana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ambapo waliwasilisha changamoto zao, ikiwemo tatizo la ajira kwa walimu.
Mwl. Kaheza ameongeza kuwa kabla ya muda huo wa siku 45 kumalizika, watakuwa wakifanya vikao vya mara kwa mara na Serikali ili kufuatilia hatua zinazochukuliwa katika kushughulikia changamoto hiyo.
Aidha, ameeleza kuwa iwapo walimu wote wasiokuwa na ajira watapata nafasi za kazi, basi Umoja wa NETO hautakuwa na sababu ya kuendelea kuwepo, kwani lengo lao limekuwa ni kuhakikisha wanapata ajira.
Leave a Reply