Shamira ahimiza vijana kujiandikisha daftari la kudumu la mpiga kura

Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti vitatu Bara Ndg. Shamira Mshangama afanya ziara Mkoani Rukwa kwa lengo la kuhamasisha vijana kushiriki katika zoezi la uandikishaji na uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura, zoezi hilo lililoanza tarehe 12- 18 Januari.

Shamira akiwa na wajumbe wa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Rukwa inayoongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Comrade Albert Kipele, Mbaraza wa Taifa Ndg. Jerome, pamoja na wajumbe wengine ngazi ya mkoa na Wilaya ya Sumbawanga walipita kwenye vijiwe vya vijana waendesha boda boda na kufanya mkutano nao kwa lengo la kuwapa elimu juu ya zoezi la uandikishaji ambalo tayari limeanza kwenye baadhi ya mikoa ya Nyanda za juu kusini.

Mwisho, walisikiliza na kujadili kwa pamoja kero za vijana waendesha boda boda, kugawa reflector na kujaza mafuta kwa maafisa usafirishaji hao.

“Vijana tuna haki ya kupiga kura kuchagua viongozi na sisi kuchaguliwa kuwa viongozi, hivyo pamoja na ratiba ngumu tulizonazo tusiache kwenda kujiandikisha na kuwasisitiza vijana wengine kwenda kujiandikisha”. Alisisitiza

{“data”:{“infoStickerId”:””,”activityName”:””,”playId”:””,”enter_from”:”enter_launch”,”stickerId”:””,”product”:”retouch”,”imageEffectId”:””,”filterId”:””,”pictureId”:”EA6EBBE8-BE4F-420E-B3B2-4A563FAB8E2F”,”os”:”ios”,”appversion”:”5.4.1″},”tiktok_developers_3p_anchor_params”:”{\”filter_id\”:[],\”client_key\”:\”awgvo7gzpeas2ho6\”,\”template_id\”:\”\”}”,”source_type”:”hypic”}