Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa (Viti Vitatu bara) Ndg. Shamira Mshangama ameshiriki kwenye ziara ya uzinduzi wa maadhimisho ya siku 7 za matukio mbalimbali ya UVCCM kusherehea miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi. Uzinduzi huo umefanyika katika Kata ya Mkwaja, wilaya ya Pangani, mkoani Tanga.

Katika maadhimisho hayo ndugu @shamiramshangama alipandisha bendera kwa wajumbe wa Mashina na kwenye maskani za Maafisa Usafirishaji ( boda boda) huku akiwa na ujumbe wa kuhamasisha vijana na wananchi wote wenye vigezo, kujitokeza kujiandikisha au kwenda kuboresha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura kuanzia tarehe 13/2/2025.

Shamira pia alitembelea kambi ya vijana wa itifaki na kukabidhi pesa kwa Viongozi wa UVCCM Wilaya ya Pangani kwa lengo la kuwezesha mahitaji muhimu ya vijana wa itifaki 230.

Mwisho, Shamira kwa kushirikiana na UVCCM Pangani walitoa tamko la kuunga mkono maadhimio ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM wa kuwapitisha wagombea wa nafasi za Urais kwa Tanzania na Zanzibar pamoja na mgombea wa nafasi ya Umakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mkutano wa hadhara.




Leave a Reply