Simba yafungiwa mechi 1 CAF, yapigwa faini ya 101m

Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) limeifungia klabu ya Simba kucheza mechi moja ya CAF bila mashabiki na kulipa kiasi cha dola 40,000 sawa na Tsh milioni 101 kutokana na vurugu zilizojitokeza katika mchezo wa kombe la shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien uliopigwa Disemba 15, 2024 simba ikiondoka na ushindi wa mabao 2-1.

Taarifa Kwa Umma kuhusu faini kutoka CAF

Kwa maamuzi hayo klabu ya Simba imesitisha mauzo ya tiketi ya mchezo dhidi ya CS Constantine na mashabiki ambao wameshanunua tiketi, tiketi hizo zitatumika kwenye mchezo ujao wa robo fainali.