Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Singida Kupitia Kubonanza la Michezo Wilayani Mkalama Imewataka Wananchi Kuepuka Vishawishi vya Rushwa hasa Kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwaka huu.
Bonanza hilo ambalo limewaleta Pamoja Wazazi na Wanafunzi kutoka Shule Mbalimbali Wilayani Mkalama limehurudhiwa na Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali ambaye Amewataka Wananchi wilayani Humo Kuikataa Rushwa kwani inakosesha Haki kiasi cha Kurudisha Nyuma Maendeleo.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoa wa Singida Sipha Mwanjala Amesema Elimu ya Rushwa inayotolewa kwa Wanafunzi itawaandaa kuwa Watumishi wa Umma Wazuri wa Baadae Huku Mkuu wa Taasisi hiyo Wilaya ya Mkalama akiwaonya Watia nia juu ya Vitendo vya Rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Baadhi ya Washiriki katika Bonanza Hilo wamesema Elimu waliyoipata itawasaidia kupata Viongozi wazuri mwaka huu na Kwamba hawapo tayari Kupokea Zawadi za Wagombea wanazozitoa ili waweze kuwachagua.
Leave a Reply