Tanzania Ya Pili Kwa Kiwango Cha Chini Cha Rushwa EAC

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, akiwasilisha taarifa ya mwaka ya utendaji TAKUKURU kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amebainisha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya pili kwa kuwa na kiwango cha chini zaidi cha vitendo vya rushwa kati ya nchi 10 za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Taarifa hiyo imetolewa kwa kutumia kiashiria cha The Corruption Perceptions Index (CPI) cha Transparency International. Chalamila alieleza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali katika kupambana na rushwa, huku akisisitiza kuwa bado kuna changamoto zinazohitaji juhudi zaidi ili kufikia jamii isiyo na rushwa na kuimarisha ufanisi wa taasisi za umma.