Serikali kupitia Wizara ya Afya imeutangazia Umma wa Watanzania na Dunia kwa ujumla kuwa baada ya siku 54 tangu kutangazwa kuwepo kwa ugonjwa wa Marburg mkoani Kagera imefanikiwa kudhibiti ugonjwa huo.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama Machi 13, Mwaka huu wilayani Biharamulo imeeleza kuwa tangu mgonjwa wa mwisho kufariki ni siku 42 zimepita na hapajagundulika mgonjwa yeyote.
Jenista ameipongeza serikali inayoongozwa na Rais Samia kwa kuimarisha huduma za Afya na wataalamu ambao wamesaidia kwa kiasi kikubwa katika mapambano ya ugonjwa huu.
Amesema kuwa zaidi ya watu 281 waliwekwa karantini baada ya kutengamana na wahisiwa wa Marburg na baada ya kufanyiwa vipimo hawakukutwa na ugonjwa huo.
Katika hatua nyingine Jenista amesema kuwa serikali imedhamilia kujenga wodi ya maalumu ya magonjwa ya mlipuko katika hospitali ya wilaya ya Bijharamulo Pamoja na kituo cha kuzalishia Oxygen.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwassa ameipongeza serikali kwa namna ilivyopambana na ugonjwa huu huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na magonjwa ya mlipuko.
Aidha Mbunge wa jimbo la Biharamulo Maghari Mhandis Ezra Chiwelesa ameiomba serikali kuboresha miundombinu ya hospitali ya wilaya huku diwani wa kata ya Ruziba ambayo ndo kata iliyobainika na ugonjwa huo ambaye ameeleza kuwa wananchi wanaendelea na shughuli zao baada ya hali kutengamaa.
Leave a Reply