Uwiano wa madaktari bingwa nchini Tanzania umeimarika kwa kiasi kikubwa, huku daktari mmoja bingwa akihudumia wagonjwa 4,000 kwa sasa.
Hayo yamesemwa leo, Juni 3, 2025, Bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama, wakati akijibu hoja za wabunge.
Mhe. Mhagama amefafanua kuwa mafanikio haya ni makubwa, akitolea mfano baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ambapo daktari bingwa mmoja huhudumia wagonjwa 25,000.
Hata hivyo, licha ya hatua hii nzuri, Mhe. Mhagama amesisitiza kuwa ni muhimu jitihada za kuongeza watumishi wa afya ziendelee kufanyika ili kuboresha zaidi huduma za afya kwa Watanzania.
Leave a Reply