Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Mhe. Cleopa David Msuya, Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea leo Mei 7, 2025 katika hospitali ya mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa Matibabu ya ugonjwa wa Moyo.
Rais Samia ameeleza kuwa Hayati Cleopa David Msuya ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa Matibabu ndani na nje ya nchi ikiwemo katika hospitali ya moyo ya Jakaya Kikwete, Mzena na Jijini London Uingereza.
Rais Samia ametangaza siku saba (7) za Maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia tarehe 7 hadi 13, Mei 2025.
Leave a Reply