Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limeeleza kuwa tsh. Milioni 200 ambayo ni fedha ya ubingwa wa Kombe la CRDB msimu wa 2024/25 ilikatwa ilikulipia madeni mbalimbali ya klabu hiyo ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni.
“Tumemsikia Meneja Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC kupitia vyombo vya habari akidai kuwa klabu yao inaidai TFF Tsh. 200,000,000/= (Milioni Mia Mbili ) ambayo ni zawadi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB.
“Tunapenda kutoa ufafanuzi kuwa TFF ndiyo inayoidai klabu hiyo. Young Africans SC iliomba kwa barua fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni,” taarifa ya TFF Imeeleza.
TFF wamefafanua zaidi kuwa Yanga waliomba kwa barua kuwa fedha zao za zawadi katika mashindano mbalimbali zikatwe kulipia malipo wanayotakiwa kulipa kwa TFF ikiwemo ada za wachezaji wa kigeni.
Klabu ya Yanga imeandikia barua na TFF ikiombwa kutuma mtaalamu wao wa fedha kesho saa 4 asubuhi kuhakiki deni la klabu hiyo akiwa na vielelezo vyote katika Ofisi za TFF.
Leave a Reply