The Weeknd Maarufu Kuliko Drake Na Justin Bieber.

Kwa Mujibu Wa Luminate (Global Export), Inayoangazia Umaarufu Na Mafanikio Ya Msanii Nje Ya Nchi Yake, Imemtaja Muimbaji @theweeknd Kama Msanii Maarufu Zaidi Duniani Kwa Sasa Kutoka Canada (Most Popular Artist In The World Currently From Canada).

Hii Yote Ni Kutokana Na Mafanikio Ya Kazi Zake, Ikiwemo Kukusanya Streams Zaidi Ya Bilioni 13 Kwa Mwaka Pamoja Na Nyimbo Zake Maarufu Kama ‘Blinding Lights’ Ambao Ndio Wimbo Wenye Streams Nyingi Zaidi Spotify. Lakini Pia Ziara Yake Ya ‘After hours Till Dawan’ Kuingiza Zaidi Ya $350M (Tsh BILIONI 943.2/=).

Vigezo hivi vinamfanya The Weeknd awe mbele ya wasanii wengine wakubwa wa Canada kama Drake na Justin Bieber.

Sio Hivyo Tu, Mwaka 2023 Guinness World Records Walimtaja The Weeknd kuwa ndiye msanii maarufu zaidi duniani (Most Popular Artist on The Planet) Akiweka rekodi kubwa mbili kwenye Kitabu hicho cha Kumbukumbu na matukio ya dunia, (Kuwa Maarufu, Na Kuwa Msanii Wa Kwanza Kufikisha Monthly Listeners Milioni 100 Spotify Duniani).

JE, Unakubaliana Nao Kwa Vigezo Hivyo Kuwa The Weeknd Ndio Msanii Wa Canada Maarufu zaidi Duniani ⁉️